Fitness Empire

ZIJUE FAIDA ZA KULA MAYAI YA KUCHEMSHA


{YA KUKU WA KIENYEJI}
MAYAI yana umuhimu na faida kubwa sana kwenye afya ya mwili wako,kwani yana vitu vingi sana kiujumla hasa kwenye kila kinachoundwa ndani yai ni faida kwa mwili wa binadamu. Mayai yana Vitamin A,K,E,D,K vitamin B6 , B12 na si hivyo tu bali kwenye mayai pia kuna folic Acid, magnesium, omega 3s fatty na copper

MAYAI yanayopendekezwa Zaidi kwa watumiaji ni mayai ya kienyeji ,Ndiyo sahihi Zaidi kutokana na yasiyoyakienyeji huwa na muunganiko wa madawa mengi sana katika ukuaji na ukuaji wa kuku hadi kufikia UTAGAJI.Mayai Ya kuku wa kienyeji ni mazuri Zaidi kwa mtumia kwasababu kila kitu ni asilia {kula mayai 2 hadi 3 kwa siku kila siku { ya kuku wa kienyeji }

Ulaji wa mayai 2- 3 kwa siku huwa na faida kubwa Zaidi ndani ya mwili na afya yenyewe kiujumla,angalia muda na hakikisha kila siku unakula mayai yaliyochemshwa.

FAIDA ZAKE NI HIZI HAPA :
1:husaidia kuzuia mashambulizi ya magonjwa ya KANSA na INI
2:husaidia sana katika kupunguza uzito
3:kusaidia kuimarisha afya ya ngozi na kungarisha nywele
4:Husaidia kupata usingizi mzuri
5:Ni chanzo kizuri cha protini mwili pia husaidia kuondoa matatizo ya macho