Fitness Empire

ZIJUE FAIDA ZA GREEN TEA

GREEN TEA ni moja kati ya vitu vinavyoboresha afya Zaidi,Yawezekana unatumia vinywaji vingi katika mfumo wako wa maisha ya kila siku asubuhi na jioni kwa ajili ya kuweka afya vizuri .lakini si mara zote unafahamu umuhimu na kujua nini unakunywa na faida zake kwa pamoja. Ni vizuri Zaidi kufahamu kiundani Zaidi juu ya kile unachokunywa na kuelewa faida na hasara zake kiujumla ili kujua kipi ni bora Zaidi kwa afya mwili wako.

Zifuatazo ni faida za kutumia GREEN TEA katika mfumo wako wa kila siku ili kuimarisha afya yako Zaidi

1: Huzuia maambukizi shambulizi kwenye INI
2:Huzuia maambukizi ya KANSA
3:Husaidia kungarisha na kukuza nywele
4:Huimarisha na kungarisha ngozi
5: Husaidia kuondoa baridi na mafua
6: Hupunguza kiwango cha stress/msongo wa mawazo
7: Husaidia kuimarisha MENO

8: husaidia kupambana na obesity kwa kuzuia movement ya glucose kuelekea kwenye fat cells

9: inasaidia kupambana na Allegies

10: inasaida kwenye suala zima la kupunguza uzito kwa kusaidia kuchoma mafuta mwilin na kurahisisha mmeng’enyo wa chakula

11: inasaidia kulinda meno na kuvunjika vunjika,kwa kuyakinga na bakteria waharibifu


NI MUDA GANI NI SAHIHI WA KUNYWA GREEN TEA ?
Katika vitu vya kuzingatia unapokunywa green tea lazima uzingatie wakati sahihi wa kunywa
1: Baada ya kifungua kinywa – Ni muhimu kunywa green tea baada ya kupata kifungua kinywa
2: Nusu saa kabla ya mazoezi– green tea inasaidia katika kupunguza mafuta mwilini
3: Saa moja kabla/baada ya mlo wa chakula – Ni vizuri kunywa saa moja kabla /baada ya mlo
4: Nusu saa kabla ya kulala – Ni vizuri pia kunywa nusu saa kabla ya kulala ili kuifanya iiweze kufanya kazi mwili ukiwa umetulia vizuri